Ingia / Jisajili

Karibu Mkombozi Wangu

Mtunzi: Anga Anselim
> Mfahamu Zaidi Anga Anselim
> Tazama Nyimbo nyingine za Anga Anselim

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio | Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Anga Anselim

Umepakuliwa mara 49 | Umetazamwa mara 106

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
Karibu Mkombozi wangu ukae ndani yangu, Nira ya Upendo na Amani ya kweli. Karibu kwangu Bwana Yesu nipate heri kweli, Ili nishiriki furaha ya Mbinguni. Njoo kwangu Bwana, Njoo nitakase, nipate uzima uzima wa milele. 1. Ambatana na Moyo wangu, shikamana na mwili wangu; Njoo Bwana, Njoo kwangu, nipate uzima. 2. Niangazishe njia yangu, Giza totoro litoweke; Njoo Bwana Njoo kwangu, nipate uzima 3. Niondoke huku porini, Ma'na simba wanizingira; Njoo Bwana, Njoo kwangu, nipate uzima. 4. Niwe mwanga kwa Majirani, Niwe nuru kwa Mataifa; Njoo Bwana, Njoo kwangu, nipate uzima. 5. Natamani Makao yako, Niwe Nawe Milele yote; Njoo Bwana, Njoo kwangu, nipate uzima.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa