Mtunzi: N. E. Kisima
> Tazama Nyimbo nyingine za N. E. Kisima
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio | Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela
Umepakuliwa mara 16,052 | Umetazamwa mara 26,492
Download Nota Download Midi1. a) Ee Mwokozi ninakukaribisha uje kwangu uwe nami daima ni wewe uliye utimilifu wewe ndiwe Kristo Mwana wa Mungu
b) Ndiwe njia ukweli na uzima nuru halisi ishindayo giza, ukanipe uzima wa milele ndio kuwa na wewe maishani
CHORUS
Karibu kwangu (mwokozi) Ee Mwokozi uje kwangu (uje mwokozi)
Karibu kwangu (mwokozi) Ee Mwokozi uwe nami
2. a) Unijaze hekima ile kuu uliyokuwa nayo Ee Mwokozi nikaishi upendo na utii na unyenyekevu maishani
b) Ukanipe akili ile kuu nikaseme karika mambo yote Baba mapenzi yako yatimizwe siku zote maishani mwangu
3. a)Maumbo ya mkate na divai fumbo kuu hilo la Ekaristi ndimo ulimoacha ukumbusho wa kujitoa kwako tuokoke
b) Sema neno tu nasi tutapona kwani wewe u neno wake Baba kwa neno lake Baba tutaishi na wewe u neno wake Baba
4. a)Ukanipe na usafi wa moyo nikamwone Mungu Baba milele ndiyo hamu niliyo nayo mimi kuonana nae uso kwa uso
b) Utukuzwe Mungu Baba muumba nawe mwana mwokozi wa dunia nawe roho mtakatifu milele hata milele. Amina