Mtunzi: André Makanga
> Mfahamu Zaidi André Makanga
> Tazama Nyimbo nyingine za André Makanga
Makundi Nyimbo: Shukrani | Tenzi za Kiswahili | Zaburi
Umepakiwa na: André Makanga
Umepakuliwa mara 9 | Umetazamwa mara 19
Download Nota Download MidiKILA MWENYE PUMZI
Kiitikio: Kila mwenye pumzi, na amsifu Bwana Mungu
Msifuni (Mungu) msifuni, katika patakatifu pake
Msifuni (Mungu) msifuni, katika anga la uweza wake
Msifuni Mungu wetu (kweli) imbeni utukufu wake
Msifuni Mungu wetu (kweli) imbeni utukufu wake.
1. Msifuni Mungu (x2) kwa matendo yake makuu
Msifuni Mungu (x2) kwa wingi wa ukuu wake
Msifuni kwa baragumu, msifuni kwa kinanda
2. Msifuni Mungu (x2) kwa kinubi na zeze
Msifuni Mungu (x2) filimbi na matoazi
Msifuni kwa kucheza, pigeni kelele za shangwe.
Hitimisho
Haya njooni wote, tumsifu Bwana Mungu (x2)
Haya njooni kwa shangwe, tumsifu Bwana Mungu (x2)
Anastahili kupewa sifa na utukufu milele yote
Enzi mamlaka vyote ni vyake, yeye ni Mungu wetu daima.
Anastahili kupewa sifa na utukufu milele yote
Enzi mamlaka vyote ni vyake, yeye ni Mungu wetu daima.