Mtunzi: Br. Emmanuel Mwita, Ofmcap.
> Mfahamu Zaidi Br. Emmanuel Mwita, Ofmcap.
> Tazama Nyimbo nyingine za Br. Emmanuel Mwita, Ofmcap.
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: Emmanuel Mwita
Umepakuliwa mara 384 | Umetazamwa mara 1,470
Download Nota Download MidiKIMYA NAMNGOJA MUNGU
1. Nafsi yangu yamngoja, Mungu peke yake kwa kimya, wokovu wokovu wangu, hutoka kwake;
Yeye tu ndiye mwamba, mwamba wangu na wokovu wangu, ngome yangu ngome yangu, sitatikisika sana.
Kimya kimya nafsi yangu, yamngoja Mungu, kimya kimya yamngoja, Mungu peke yake x2
2. Nafsi yangu umngoje Mungu, Mungu peke yake kwa kimya, tumaini tumaini langu, hutoka kwake;
Yeye tu ndiye mwamba wangu, na wokovu wangu, ngome yangu ngome yangu, sitatikisika sana.
3. Kwa Mungu wokovu wangu, na utukufu wangu, mwamba wa nguvu zangu, na kimbilio langu ni kwa Mungu;
Enyi watu mtumaini, mtumaini siku zote, ifunueni mioyo yenu, Mungu ndiye kimbilio letu.