Mtunzi: J. Darwall
Makundi Nyimbo: Kristu Mfalme | Pasaka | Tenzi za Kiswahili
Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela
Umepakuliwa mara 1,234 | Umetazamwa mara 3,749
Download Nota Download Midi1. Kristo ndiye jiwe kuu la pembeni; tumejengwa kwake sasa kwa imani: mapenzi yake ni makuu tunayatumaini tu.
2. Sana na zipae nyimbo zetu hizi, kanisa ijae, sifa za mwokozi, jina lake litukuzwe, sifa zake na zipazwe.
3. Karibia hapa ewe mungu wetu; ridhia kutupa hapa juu yetu baraka zitufaazo; zaidi ya tuombazo.
4. Hapa natupate neema ya mbingu; hapa tusiache kumwimbia mungu; hata tutakapokwenda kwake aliyetupenda.