Maneno ya wimbo
Kiitikio
Kwa Bwana kuna fadhili (II &IV fadhili) na kwake kuna ukombozi mwingi x2
Maimbilizi
1. Ee Bwana, toka vilindini nimekulilia,
Bwana, uisikie sauti yangu.
Masikio yako na yaisikilize
Sauti ya dua zangu.
2. Bwana, kama Wewe ungehesabu maovu,
Ee Bwana, nani angesimama?
Lakini kwako kuna msamaha
Ili Wewe uogopwe.
3. Nimemngoja Bwana,
roho yangu imemngoja,
Na neno lake nimelitumainia.
4. Nafsi yangu inamngoja Bwana,
Kuliko walinzi waingojavyo asubuhi,
Naam, walinzi waingojavyo asubuhi,
Ee Israeli, umtarajie Bwana.
5. Maana kwa Bwana kuna fadhili,
Na kwake kuna ukombozi mwingi.
Yeye atamkomboa Israeli
Na maovu yake yote.
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu