Ingia / Jisajili

Kwa Nini Wanipiga ?

Mtunzi: Mmole G.
> Tazama Nyimbo nyingine za Mmole G.

Makundi Nyimbo: Juma Kuu | Kwaresma | Matawi

Umepakiwa na: Vitus Chigogolo

Umepakuliwa mara 4,921 | Umetazamwa mara 9,265

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kama nimesema vibaya toa ushahidi wa neno baya bali kama nimesema vema kwanini wanipiga? X2

1.       Pilato alimhukumu Yesu ingawa hakuona makosa kwake aliwaogopa Wayahudi na kubembeleza urafiki wa Kaisari

2.       Ndugu yangu tafakari kwa makini mamlaka ulopewa na wenzio unayatumia ipasavyo au waumiza wenzako kama Pilato

3.       Askari usalama wa raia acheni kuwadhulumu raia na kusingizia watu kesi mnasababisha uvunjaji wa sheria

4.       Mahakimu na mabingwa wa sheria haifai kuipotosha sheria maskini wajane na yatima mnawanyang’anya haki zao hukumuni

5.       Waganga wakunga na wauguzi tibuni bila kudai zawadi watu masikini na yatima wanahangaika vitandani hadi kufa

6.       Wanandoa tunzeni ahadi zenu kupendana katika shida na raha pia kuwalea wana katika njia impasayo Mkristo

7.       Utoaji wa mimba bila sababu nakutupa watoto majalalani nikuto ujali utu wa mtu wenu na kuwahukumu kifo wasio na kosa

8.       Dunia yetu inawaka moto amani yetu imeshatoweka vita vyatawala kina kona kisa ni tama ya mali na madaraka


Maoni - Toa Maoni

EMMANUEL MARWA Mar 26, 2024
Sina neno kwa sasa

Toa Maoni yako hapa