Mtunzi: A.Family
> Mfahamu Zaidi A.Family
> Tazama Nyimbo nyingine za A.Family
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: Aloyce Family
Umepakuliwa mara 0 | Umetazamwa mara 0
Download Nota Download MidiWewe Bwana umekuwa makao yetu×2 kizazi baada yakizazi kizazi baada ya kizazi×2
1..Wamrudisha mtu mavumbini, usemapo rudini enyi wanadamu, maana miaka elfu machoni pako nikama siku ya jana ikiisha kupita, na kama kesha la usiku.
2..Wawagharikisha huwa kama usingizi Asubuhi huwa kama majani yameayo Asubuhi yachipuka nakumea, jioni yakatika na kukauka.
3..Basi utujulishe kuzihesabu siku zetu tujipatie moyo wahekima Ee Bwana urudi hata lini, uwahurumie watumishi wako.
4..Utushibishe Asubuhi kwa fadhili zako nasi tutashangilia nakufurahi siku zetu zote, na uzuri wa Bwana Mungu wetu uwe juu yetu, na kazi yamikono yetu uithibitishe.