Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Watakatifu | Zaburi
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 683 | Umetazamwa mara 2,988
Download Nota Download MidiMalaika wa Bwana hufanya kituo
Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa x3
1.Nitamhimidi Bwana kila wakati,
sifa zake zi kinywani mwangu daima
Katika Bwana nafsi yangu itajisifu,
wanyenyekevu wasikie wakafurahi
2.Mtukuzeni Bwana pamoja nami,
tuliadhimishe jina lake pamoja
Nalimtafuta Bwana akanijibu,
akaniponya nazo hofu zangu zote
3.Wakamwelekea macho wakatiwa nuru,
wala nyuso zao hazitaona haya
Maskini huyu aliita Bwana ’kasikia,
akamwokoa katika taabu zake zote