Ingia / Jisajili

Mama Maria

Mtunzi: Boniface Katiku
> Mfahamu Zaidi Boniface Katiku
> Tazama Nyimbo nyingine za Boniface Katiku

Makundi Nyimbo: Mama Maria

Umepakiwa na: Boniface Katiku

Umepakuliwa mara 158 | Umetazamwa mara 567

Download Nota
Maneno ya wimbo
1. Mama Maria mwombezi wetu, utuombee kwake mwanao, atusamehe makosa yetu, tuwe salama tubarikiwe, tuwe nadhifu atupokee.. Twaliimba jina ee mama Maria tumejaa furaha ee Mwombezi wetu, tunakuja kwako mwingi wa Rehema tuombee mama wakosefu sisi 2. Twakusalimu mama Maria, mwenye bidii kutuombea, sisi wanao tunakuomba, maisha yetu ni wasiwasi, maisha yetu ni dukuduku. 3. Uliyepalizwa mbinguni juu, kafanywa kuwa wetu mfalme, we nyota yenye kuangaza kote, uzifikishe sala zetu kwake, maombi yetu umfikishie. 4. We' ua nzuri linametameta, linalonukia kwa wema wake, utuwezeshe kufika huko, huko mbinguni maskani yetu, penye makao na ya milele.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa