Ingia / Jisajili

Mimi Ni Mtumishi Wake Bwana

Mtunzi: Fr. Gregory F. Kayeta
> Tazama Nyimbo nyingine za Fr. Gregory F. Kayeta

Makundi Nyimbo: Majilio | Mama Maria

Umepakiwa na: Vusile Silonda

Umepakuliwa mara 6,290 | Umetazamwa mara 13,603

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Mimi ni mtumishi wake Bwana, nitendewe ulivyonena x 2
Nitendewe, ulivyonena, mimi ni mtumishi wa Bwana, mimi ni mtumishi wa Bwana, nitendewe ulivyonena

 1. Salamu uliyejaa neema, Bwana yu pamoja nawe.
   
 2. Usiogope Maria, Mungu kakupendelea.
   
 3. Tazama utapata mimba utamzaa mwana, utamwita jina lake Yesu.
   
 4. Huyu atakuwa mkuu, ataitwa mwana wa aliye juu.
   
 5. Bwana Mungu atampa kiti cha enzi, cha Baba yake Daudi.
   
 6. Ataitawala nyumba ya Yakobo hata milele, ufalme wake hautakuwa na mwisho.
   
 7. Roho Mtakatifu atakushukia, na nguvu ya yule aliye juu itakutia kivuli.
   
 8. Ndiyo maana huyo mtoto atakuwa mtakatifu, huyo ataitwa mwana wa Mungu.

Maoni - Toa Maoni

Clemence bayona Dec 10, 2019
Naomba huu wimbo "mimi ni mtumishi wake bwana nitendewe ulivyonena"

peter anderson Aug 19, 2019
bwana asifiwe. naomba wimbo wa MIMI NI MTUMISHI WAKE BWANA. naomba audio kwa whatsapp 0657461362 ama email peteranderson938@gmail.com

Toa Maoni yako hapa