Mtunzi: Rev. Fr. L. Malema
Makundi Nyimbo: Miito
Umepakiwa na: Vusile Silonda
Umepakuliwa mara 3,601 | Umetazamwa mara 7,468
Download Nota Download Midi
FR. L. MALEMA.
Mimi nimewachagua ninyi duniani, mimi nimewachagua duniani
(Ili mpate kwenda kuzaa matunda, na matunda yenu yadumu, yadumu siku zote ) X2
1. Si ninyi mlio nichagua mimi, bali ni mimi niliowachagua ninyi.
2. Nami nimewachagua kwenda kuzaa matunda, na matunda yenu yadumu/ ili kwamba lolote mumwombalo Baba, kwa jina langu awape.
3. Iwapo ulimwengu ukiwachukia/ mjue kwamba umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi.
4. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungeliwapenda/ lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi nimewachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu utawachukia.