Ingia / Jisajili

Misa Mtakatifu Veronika

Mtunzi: Kennedy Mulwa
> Tazama Nyimbo nyingine za Kennedy Mulwa

Makundi Nyimbo: Misa

Umepakiwa na: Kennedy Mulwa

Umepakuliwa mara 4,631 | Umetazamwa mara 11,965

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

MISA MTAKATIFU VERONIKA

Utuhurumie

(S: Ewe Bwana tuhurumie

 W: Ewe Bwana tuhurumie) x3

(S: Ewe Bwana

 W: Ewe Bwana) x2

Ewe Kristu…

Ewe Bwana…

Utukufu

T: Utukufu kwa Mungu juu mbinguni

W: Na amani duniani kwao watu wenye mapenzi mema

Tunakusifu, tunakuheshimu, tunakuabudu, tunakutukuza x2

Tenor & Bass- (Bwana) Sifu Bwana, kuheshimu, tunakuabudu (B:Bwana)  tunakutukuza x2

  1. Baba tunakushukuru, kwa ajili ya utukufu wako
  2. Ewe Mungu ni mfalme, wa mbinguni, Mungu Baba Mwenyezi
  3. Bwana Mungu mwanakondoo, wake Mungu ni mwana wake Baba
  4. Ewe mwenye kuziondoa, dhambi za dunia tuhurumie
  5. Ewe mwenye kuketi kuume, kwake Mungu Baba, tuhurumie
  6. Pekee yako ni Mtakatifu, pekee yako ni Bwana Yesu Kristu
  7. Pia na Roho Mtakatifu, katika utukufu wake Baba

Nasadiki

  1.  Nasadiki kwa Mungu mmoja

 Ndiye Baba yetu Mwenyezi

Mwumba mbingu pia dunia

Nasadiki kwa Yesu Kristu

Nasadiki, nasadiki x2

  1.  Mwana wa pekee wa Mungu-

       Mwenye kuzaliwa kwa Baba-

       Akapata mwili kwa Roho-

       ‘Kazaliwa naye Bikira

  1. Kisha yeye ‘kasulibiwa-

     Kwa amri ya Ponsio Pilato-

     Kwa ajili yetu ‘kateswa-

     Akafa na akazikwa-

  1. ‘Kafufuka katika wafu-

       ‘Kapaa juu mbinguni-

       Ameketi kuume kwake-

       Mungu Baba yetu mwenyezi-

  1. Ndipo atakapotokea-

      ‘Kuhukumu wazima na wafu-

       Kwake Roho Mtakatifu-

       Kwa Kanisa la Katoliki-

  1. Ushirika wa watakatifu-

      ‘Ondoleo la dhambi zetu-

       Nangojea ufufuko wa  mwili-

       Na uzima wa milele

Mtakatifu

Mtakatifu x3 Bwana Mungu

Mtakatifu x3 wa majeshi

Mbingu na dunia zimejaa utukufu wako Ewe Bwana Mungu

Hosana juu, Hosana juu, Hosana mbinguni (Hosana) x2

Mbarikiwa ni yule ajaye kwa jina lake Bwana

Hosana juu, Hosana juu, Hosana mbinguni (Hosana) x2

Baba Yetu

{S: Baba yetu wa mbinguni

 W: Jina lako litukuzwe} x2

  1. ‘falme wako uje kwetu, utakalo lifanyike, duniani kama mbinguni.
  2. Tupe leo mkate wetu, mkate wetu wa kila siku, utakalo lifanyike.
  3. Tusamehe dhambi zetu, kama vile twawasamehe, nao waliotukosea.
  4. Situtie majaribuni, maovuni utuopoe, utakalo lifanyike.
  5. Kwa kuwa ‘falme ni wako, nazo nguvu na utukufu, vyote vyako hata milele.

Mwanakondoo

{Mwanakondoo wa Mungu ee

(B: Ee Mwana) Ee Mwana, (B: Ee Mwana) wa Baba} x2

Uondoaye dhambi zetu tunakuomba utuhurumie x2

{Mwanakondoo wa Mungu ee

(B: Ee Mwana) Ee Mwana, (B: Mwana) wa Baba} x2

Uondoaye dhambi zetu tunakuomba utuhurumie x2

{Mwanakondoo wa Mungu ee

(B: Ee Mwana) Ee Mwana, (B: Mwana) wa Baba} x2

Uondoaye dhambi zetu tunakuomba utupe amani x2

Nyimbo nyingine za mtunzi huyu

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa