Mtunzi: John Ondege
Makundi Nyimbo: Mama Maria
Umepakiwa na: Boniface Muyonga
Umepakuliwa mara 272 | Umetazamwa mara 1,101
Download Nota
Download Midi
Maneno ya wimbo
Moyo mtakatifu wa mama Maria, sisi
wana wako tunalia mbele ya uso wako.
(mama-mama-mama, mama utuombee x2)
1. Umebarikiwa mama wa Mungu , mama wa
mwokozi mama wa yesu, utuombee - mama
mwenye huruma.
2. Uwinguni juu unapoketi, na wanao Yesu,
unatawala, utuombee - mama utuongoze.
3. Adui shetani ametupana, utukingie na hila zako,
utuombee - mama mwenye huruma.
4. Na siku ya mwisho usiwe mbali, kufa pekee yetu
usikubali mama mwenye huruma utuombee
5. Mama wetu bora tunakusifu, na huko mbinguni
wakuheshimu, utuunganishe - ee mama mwe-ma.