Ingia / Jisajili

Mshukuruni Mwokozi

Mtunzi: Joseph Makoye
> Tazama Nyimbo nyingine za Joseph Makoye

Makundi Nyimbo: Shukrani

Umepakiwa na: Alex Rwelamira

Umepakuliwa mara 856 | Umetazamwa mara 1,092

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
Mshukuruni Mwokozi enyi mataifa pigeni vigelegele pigeni makofi X2

Tangazeni rehema zake leo asubuhi semeni ya kuwa Bwana ni mwenye adili X2

1. Njoni tumwimbie Bwana mwamba wa wokovu wetu mikononi mwake zimo bonde za dunia bahari ni yake ndiye aliyeumba na mikono yake ilituumba sisi

2. Bwana ametamalaki mataifa watetema ameketi juu ya makerubi mbinguni yeye Bwana katika Sayuni ni Mkuu katukuka juu ya mataifa yote

3. Mshangilieni Bwana mwimbieni na zaburi vinanda na baragumu vyote mvipige mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema kwa kuwa fadhili zake ni za milele

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa