Ingia / Jisajili

Mungu Alinipa Tuzo

Mtunzi: Lucas R. Masila
> Mfahamu Zaidi Lucas R. Masila
> Tazama Nyimbo nyingine za Lucas R. Masila

Makundi Nyimbo: Shukrani | Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Thomas George Mwakimata

Umepakuliwa mara 365 | Umetazamwa mara 1,437

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Mwenyezi Mungu alinipa tuzo kadiri ya uadilifu uadilifu x 2, Alinituza kwa vile mikono yangu haina hatia alinituza kwa vile mikono yangu haina hatia x 2.

Mashairi:

1 (a)  Maana nimefuata njia za mwenyezi Mungu

   (b) Wala sikujitenga na Mungu wangu kwa uovu, nimeshika maagizo yote.

2 (a) Mbele yake sikuwa na hatia nimejikinga

   (b) Mwenyezi Mungu amenituza uadilifu, yeye anajua usafi wangu.

3 (a) Wewe ni mwaminifu kwa walio waaminifu

   (b) Wewe mkamilifu kwa walio waaminifu, mkatili kwa walio waovu.

4 (a) Wewe wawaokoa walio wanyenyekevu

   (b) Ee mwenyezi Mungu wewe u taa yangu, Mungu unayefukuza giza.

Nyimbo nyingine za mtunzi huyu

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa