Ingia / Jisajili

Mungu Ananipenda

Mtunzi: Kelvin B Bongole
> Mfahamu Zaidi Kelvin B Bongole
> Tazama Nyimbo nyingine za Kelvin B Bongole

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Linus Kamarasente

Umepakuliwa mara 1 | Umetazamwa mara 0

Download Nota
Maneno ya wimbo
Yeye aliyeniumba mimi toka tumboni mwa mama yangu pasipo mimi kumuomba. Yeye aliyeniokoa toka utumwani mwa dhambi pasipo mimi kumuomba. Yeye ndiye Mungu wangu tumaini la maisha yangu, kimbilio boma langu nyakati za huzuni. Kwako naielekeza nafsi yangu ee Mungu wangu usiniache uniongoze katika kweli yako Mungu wangu mwokozi wangu. Nazo dhambi za ujana wangu usizikumbuke Mungu wangu unikumbuke kwa kadiri ya fadhili zako Mungu wangu mwokozi wangu. Najua ya kuwa mtetezi wangu yu hai na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi, na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivyo nami nisipomwili nitamuona Mungu wangu.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa