Ingia / Jisajili

Mungu Wangu Mbona Umeniacha ?

Mtunzi: V. Chigogolo
> Mfahamu Zaidi V. Chigogolo
> Tazama Nyimbo nyingine za V. Chigogolo

Makundi Nyimbo: Juma Kuu | Matawi

Umepakiwa na: Vitus Chigogolo

Umepakuliwa mara 2,631 | Umetazamwa mara 7,618

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Mungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha? Mbona umeniacha? X2

1.       a) Wote wanionao hunicheka sana hunifyonya wakitikisa vichwa vao

b)Husema umetegemee Bwana na amponye na amwokoe sasa maana apendezwa naye

2.       a) Kwa maana mbwa wamenizunguka; Kusanyiko la waovu wamenisonga;

b)Yamenizua mikono na miguu. Naweza kuihesabu mifupa yangu yote.

3.       a) Wanagawanya nguo zangu, na vazi langu wanalipigia kura.

b)Nawe Bwana, usiwe mbali; Ee Mungu wangu, fanya haraka kunisaidia.

4.       a)Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu, katikati ya kusanyiko nitakusifu.

b)Ninyi mnaomcha Bwana msifuni, enyi nyote mlio wazao wa Yakobo mtukuzeni.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa