Ingia / Jisajili

Mwachie Mungu

Mtunzi: Gitonga K. David
> Mfahamu Zaidi Gitonga K. David
> Tazama Nyimbo nyingine za Gitonga K. David

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio | Mafundisho / Tafakari | Mazishi | Moyo Mtakatifu wa Yesu | Mwanzo | Watakatifu

Umepakiwa na: DAVID GITONGA

Umepakuliwa mara 65 | Umetazamwa mara 97

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
MWACHIE MUNGU 1. Huishivyo humu duniani maisha yako kweli kama puto. Ipaayo kule angani na kupeperushwa na upepo. Maisha haya ni pandashuka, nawe umejawa na shaka. Kuna mengi hauyawezi mwachie Mungu. Njooni kwangu mnaoteseka na kulemewa nayo mizigo, nami nitawapa pumziko. Sikiza sauti ya Mungu ndugu akualika umwachie yote, (shida zako (na) maumivu (yote), nia zako na(yo) furaha. (Kwani) Mungu ndiye mweza wa yote mwachie yeye.) X2 2. Tazama ndege wa angani hawalimi kupanda wala kuvuna. Mungu mwenyewe huwalisha kwa sababu ni viumbe vyake. Wewe ni wa dhamani zaidi, nywele zako ana idadi. Mwanzo, mwisho wako ajua mwachie yote. 3. Mipango yako haiendani juhudi zako hazifuhi dafu. Marafiki wakukimbia jamaa zako wamekutenga. Hatima yako imefichika, utokako huna hakika. Mungu ndiye mwanzo na mwisho mwachie yote. 4. Mambo yanapokwenda vizuri hizo baraka zatoka kwa Mungu. Katika furaha kumbuka wema wa Mungu wakuzunguka. Yeye huyafanya mema yawe, daima yu pamoja nawe. Ndiye pekee yake Mwenyezi mwachie yote.
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa