Ingia / Jisajili

Mwamvuli wa Ukristo

Mtunzi: Dan.s.mwogoye
> Tazama Nyimbo nyingine za Dan.s.mwogoye

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Daniel .S.Mwogoye

Umepakuliwa mara 163 | Umetazamwa mara 809

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
KIITIKIO Mmejifunika mwamvuli wa ukristo lakini ndani mwenu ni upagani mtupu ndugu zangu, mlibatizwa mkamkana shetani mbona leo mwayatenda ya shetani, Imani yenu ni ile ya maigizo hakika hukumu yenu ikaribu. MASHAIRI 1.Fikirini ndugu kama mnatenda vema, na sheria ya ndoa mmeitupa mbali mwajiharalishia ndoa za kipagani. 2.Fikirini ndugu juu ya uzinzi wenu, pia ushirikina , unafiki na hila, mnafanya maovu yasiyo elezeka. 3.Mnaosaliti viapo vyenu kwa Mungu, mwajiwashia moto, tanuru la kuzimu rudini mkatubu msijeangamizwa.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa