Mtunzi: Felician Albert Nyundo
> Tazama Nyimbo nyingine za Felician Albert Nyundo
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio
Umepakiwa na: Gervas Kombo
Umepakuliwa mara 12,318 | Umetazamwa mara 21,092
Download Nota Download Midi1. Mwili wa Bwana Yesu chakula mbingu
Ni chakula cha roho chenye uzima
Hima uwe nasi Ee Bwana Yesu
Ukatushibishe chakula bora
2. Yesu alitwambia, yeye ni chakula,
Ni chakula cha Roho, chenye uzima.
Anilaye mimi, na kunywa damu,
anao uzima, wa siku zote,
Ni chakula cha Roho, chenye uzima.
3. Yesu alitwambia, kuwa tumpokee,
Ni chakula cha Roho, chenye uzima.
Sote twaamini, ni mwili wake,
Pia twaamini ni damu yake,
Ni chakula cha Roho, chenye uzima.
4. Hii ndiyo karamu, aliyotwachia,
Ni chakula cha Roho, chenye uzima.
Ee Bwana mwokozi, tunakuomba,
Kwa chakula hiki, tuimarike,
Ni chakula cha Roho chenye uzima