Mtunzi: Gabriel C. Mkude Sekulu
> Tazama Nyimbo nyingine za Gabriel C. Mkude Sekulu
Makundi Nyimbo: Miito
Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela
Umepakuliwa mara 8,392 | Umetazamwa mara 15,226
Download Nota Download MidiG. C. MKUDE.
Siyo kwamba nimekwisha fika au nimekwisha kamilika, La! La!
(bali ninakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo limeshikwa naye Kristu)x2
1. Ninaendelea mimi katika utumishi wangu nijalie nguvu Bwana wangu niyashinde haya ya dunia.
2. Nishike mkono Bwana wangu shetani asinisumbue niongoze vyema Bwana wangu niyashike majukumu yangu.
3. Nitashinda mimi nitashinda nitashinda kwa nguvu zako ninatarajia ushujaa endapo wewe utaamua.
4. Nitavikwa mimi nitavikwa nitavikwa taji ya haki sio kwa nguvu zangu mwenyewe bali kwa nguvu za Mungu Baba.
5. Aleluya nitaimba mimi nitakapo maliza safari hayo ni matarajio yangu mwisho wa hii safari yangu.