Ingia / Jisajili

Nani Mkamilifu

Mtunzi: Elias Fidelis Kidaluso
> Tazama Nyimbo nyingine za Elias Fidelis Kidaluso

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela

Umepakuliwa mara 6,096 | Umetazamwa mara 11,769

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Nani aliye mkamilifu kati yenu kama Malaika asye na dhambi awezaye kumhukumu ndugu yake x 2 
Basi jivikeni nguo tena nguo yenye mapendo na Roho nyepesi tena Roho yenye msamaha kwa ndugu zenu kama Baba wa mbinguni alivyo kwa ajili yenu x 2

  1. Msihukumu wengine, ili nanyi msije mkahukumiwa, kwa maana jinsi mnavyowahukumu wengine, hivyo ndivyo nanyi pia mtakavyohukumiwa.
     
  2. N kipimo kile kile, mtakacho kitumia kwa wengine, hicho ndicho kitakachotumika kwa Roho zenu, kuyapima matendo yenu kwa ufalme wa Mungu.
     
  3. Basi iweni wapole wenye moyo wakusamehe wengine, tena msije kuwa na Roho ngumu kama jiwe, mkijivika upendo na moyo wenye fadhila.

Maoni - Toa Maoni

Fr. Piency S. Punguti Nov 14, 2021
Napenda kumshukuru Mungu kwa karama hii nzuri aliyo kutunuku. Hongera pia kwa kuifanyia kazi karama hii njema ya uinjilishaji kwa njia ya Music Mtakatifu.

Fr. Piency S. Punguti Nov 14, 2021
Napenda kumshukuru Mungu kwa karama hii nzuri aliyo kutunuku. Hongera pia kwa kuifanyia kazi karama hii njema ya uinjilishaji kwa njia ya Music Mtakatifu.

Simon Shimba Jan 11, 2021
Mwl Elias Kidaluso unakipaji cha hali ya juu kabisa utunzi wako na upigaji kinanda ni mahili kweli kweli Mungu akuongoze

Ferdinand Makori Moriasi Oct 08, 2019
Kazi nzuri ajabu. Mungu akuongeze nguvu Elias kwenye utumwa wako.

Toa Maoni yako hapa