Ingia / Jisajili

Nasikia Sauti Ya Bwana

Mtunzi: Eric Lucas Maumba
> Mfahamu Zaidi Eric Lucas Maumba

Makundi Nyimbo: Miito

Umepakiwa na: Vusile Silonda

Umepakuliwa mara 14,157 | Umetazamwa mara 24,481

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kiitikio:

Nasikia Bwana unaniita x 2
Nichague mimi, nitakase Bwana, nichague mimi, niwe wako, niwachunge kondoo wako x 2

Mashairi:

  1. Roho inataka, kuitikia, mwili ni dhaifu, ninasongwa
    Bwana nipe nguvu kuitikia, siku zote mimi, nikupende
     
  2. Kundi lako Bwana linavutia, Bwana nipe fimbo nilichunge.
    Shetani mwovu ananyatia, Bwana nipe nguvu nimshinde.
     
  3. Mbwa mwitu nao wananyatia, Bwana nipe nguvu niwashinde.
    Niwe mchungaji na kubakia, mwaminifu kwako siku zote.
     
  4. Baba pia mwana niwatukuze, Roho Mtakatifu atukuzwe.
    Roho wako Bwana aniongoze, daima milele niwe wako.

Maoni - Toa Maoni

Robert Balama Jul 18, 2020
Huu wimbo huwa unanibariki sana , una amsha wito kutoka ndani ya Moyo

francisca kimbe Feb 10, 2020
wimbo mzuri sana unavutia hongera mungu akupe nguvu na utashi utunge mwingine

Kelvin kyamba Aug 06, 2019
Nyimbo inanibariki sana, God bless you brother.

Erick Lucas Maumba/Mkude Jul 26, 2018
Wimbo huu ni wa kwangu Erick Lucas Mkude ila kwenye wimbo huu niliamua kutumia Erick Lucas Maumba yote ni majina yangu. Ngwila ni mdogo wangu na class mate kuanzia pre form one mpaka form six pale St. Peter's Seminary tumejifunza mziki pamoja na harmony so in many cases nyimbo zetu zina mfananio wa ki harmony as brothers from the same pot of cookings. Tuyafanye yote pamoja kwa utukufu wa Mungu

Huo wimbo Nasikia Bwana Unaniita ni wa kwangu Erick Lucas Mkude (Maumba) Ngwila ni mdogo wangu inawezekana alichora somewhere ila sio wake ni wangu Jun 21, 2017
Tumwimbie Bwana Mungu wetu tungali hai

Christopher Ndaga Jun 20, 2017
kazi nzuri ila sipati njia ya kuupata wimbo wenyewe uliotungwa na Eric Lucas Maumba na kwanya iliyoimba naomba nisaidiwe

fabian mlelwa Feb 19, 2017
mungu awabaliki kazi njuli sana

Jonas Kisinini Dec 02, 2016
samahani kuna wimbo umeandikwa nasikia unaniita by ngwila , na nasikia sauti ya bwana inaniita Eric Lucas maumba, ukisiliza hizi nyimbo zinafanana na watunzi tifauti. je wimbo ni wa Nani?

Toa Maoni yako hapa