Mtunzi: J. Tobias
Makundi Nyimbo: Ndoa
Umepakiwa na: FRED KITUYI
Umepakuliwa mara 1,905 | Umetazamwa mara 4,263
Download Nota Download MidiNDOA YENU (J. TOBIAS)
Kiitikio:
Bwana na bibi harusi amkeni njoo – Mungu amawaunganisha.
Leo siku ya furaha tushangilieni – heko kweli kwa Bwana Mungu.
(Ndoa yenu (Ee!) ni takatifu, ndoa yenu itasitawi (Ee!),
Mtazaa (Ee!) matunda mema yenye baraka za Mungu.) x2
1. Mtu atamwacha babaye, atamwacha na mama yake,
Ataambatana naye mke na kuwa mwili mmoja kweli.
2. Mmekuwa mwili mmoja, Bwana Mungu mwenyewe ndiye,
Amewaunganisha pamoja, hawezi mtu kutenganisha.
3. Mtazaa matunda mema, nyumba yenu iwe ya sala,
Mkawatunze watoto wenu, kwa neno lake Mwenyezi Mungu.
4. Sisi sote tushangilie, Mungu wetu kwa mema yote,
Vigelegele tukavipige, vinanda, ngoma, vinubi piga.