Ingia / Jisajili

NI KWA NEEMA YAKO YESU

Mtunzi: Seraphin T.m.kimario
> Tazama Nyimbo nyingine za Seraphin T.m.kimario

Makundi Nyimbo: Shukrani

Umepakiwa na: Joseph Rumanyika

Umepakuliwa mara 1,539 | Umetazamwa mara 4,931

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

KIITIKIO

  • Yote uliyonijalia ni kwa neema yako tu Bwana Yesu, Hata unayonijalia ni kwa neema yako tu Bwana Yesu,
  • Na utakayonijalia ni kwa neema yako tu Bwana Yesu
  • Kweli wewe ni tumani langu daima, Tena wewe ni tegemeo langu daima,
  • Na tena wewe n kimbilio langu daima
  • (Sasa Bwana twende kwa nani )X2, (wewe unayo maneno ya uzima wa milele)X2

MAIMBILIZI

  • 1. Nikitafakari tangu kuzaliwa kwangu mpaka hivi sasa, Umenijalia mengi yaliyo mema kuliko yenye mikasa
  •      Umeniponya na magonjwa tena ya kutisha sana, hata pale palipovunjwa umengaisha tena,
  •      Sifa kwako Yesu kwa neema yako tu.

  • 2. Familia umenijalia Baba MAMA na watoto, iwe bora kama ile ya Yesu Maria na Yosefu,
  •      tukuje Mungu tukupende wewe, tukutumiki mwisho tuje kwako juu mbinguni

  • 3. Kwa neema Yako Yesu mashamba yet yamesitawi yakamea sana yakazaa sana, 
  •      Kwa neema yako Yesu samaki wengi nimewavua nilitega nyavu nikafanikiwa,
  •      Kwa neema yako Yesu shuleni hawa wamefaulu kwani ulisema shikeni elimu


HITIMISHO

  • Haya njoni wate tumshangilie Yesu, Kwani yeye ndiye jibu la maisha yetu,
  • Yeye ndiye furaha yetu wakati wa furaha, yeye ndiye mafanikio tena ndiye baraka
  • tena Yesu ndiyemfariji mwema katika shida, na katika taabu na magonjwa yeye ndiye tiba
  • (asante Yesu sifa kwa Yesu)x2

  • Nitakutumaini Yesu katika maisha yangu, nitakutegemea Yesu daima na milele,
  • Nitakuita Bwana Yesu katika maisha yangu, nitakusifu mfalme Yesu daima na milele.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa