Ingia / Jisajili

NI MUNGU TU

Mtunzi: Seraphin T.m.kimario
> Tazama Nyimbo nyingine za Seraphin T.m.kimario

Makundi Nyimbo: Shukrani

Umepakiwa na: Joseph Rumanyika

Umepakuliwa mara 679 | Umetazamwa mara 2,188

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
  • KIITIKIO
    • Anga na dunia yote ee pande zote za dunia njoni, falme na tawala zote ee makabila yote pote njoni
  • tumtukukzeni Mungu nidye Mungu, tumshukuruni Mungu ndiye Mungu, ndiye kila kitu katika maisha yetu
  • ndiye mwanzo wetu pia ndye mwisho wetu, tumtegemee Mungu ndiye Mungu, tumtumaini Mungu ndiye Mungu.


  • MAIMBILIZI
  • 1. Nikiwaza alikonitoa Mungu mpaka hapa nilipo mimi, Nikitafakari ninakoelekea hata nikapofika mimi
  •      Asubuhi ni Mungu mchana ni Mungu, jioni ni Mungu usiku ni Mungu.

  • 2.  Ona kweli yeye Mungu anatuwazia mema, kweli yeye Mungu anatuwazia mema,
  •      Shuleni wamefaulu ee, ni Mungu tu, shambani mavuno mengi ee, ni Mungu tu
  •      Mafanikio kazini ee, ni Mungu tu, na jinsi tulivyo hivi ee ni Mungu tu 

  • 3. Umetuepusha na ajali na magumu yaliyo mengi, ukatunusuru sasa baba tumekujja kukushukuru
  •      Nitakusifu Mungu milele yote, Nitakutuza Mungu milele yote

  • HITIMISHO
  • Haya njoni wote ee, tumshangilie Mungu tumpe sifa, tumsujudie yeye tumpe sifa
  • Ametujalia mengi hata tusiyoyajua, wala tusijisifie kwamba ni uwezo wetu
  • Basi tumjue sana sana Mungu, ili tuwe na Amani amani sisi.
  • ndivyo mema yatakavyotujia x2

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa