Mtunzi: Zachariah Ichingwa
> Mfahamu Zaidi Zachariah Ichingwa
Makundi Nyimbo: Shukrani
Umepakiwa na: Zacaria Ichingwa
Umepakuliwa mara 697 | Umetazamwa mara 1,976
Download Nota Download Midi1.Nimesikia nyimbo nzuri za kumsifu Mungu wangu Nimependezwa sana mimi kumwimbia Mungu wangu, waimbaji wanaziimba wachezaji wanazicheza Utukufu wake Muumba uhimidiwe siku zote
Ni raha kuimba (nyimbo) ni Raha kucheza (ngoma) Ni raha kusifu Mungu kwa nyimbo tamu tamu, Ndiye tegemeo (pekee) ndiye kimbilio (letu) chanzo cha uzima wetu ndiye ngome yetu x2
2. Malaika wanaziimba nyimbo nzuri tena tam tam wanamtukuza muumba kwa sauti za kupendeza, kwa hii lugha ya muziki asikia kuomba kwetu sauti zetu zinafika kwake Mungu wa Israeli
3. Tukimwimbia kwenye shida anatuhurumia sana ata tukiwa na huzuni yeye analeta faraja, akisikia nyimbo zetu nazo zimpendeze sana Heri neema nazo raha atazishusha kwetu sisi.
4. Tupase sauti wapendwa tutangaze sifa za bwana kwani tukifanya hi~vyo ni raha tena ni baraka, wacheza vinanda tucheze watunzi wa nyimbo tutunge wa kristu tushangilieni Mungu yuko nasi milele.