Maneno ya wimbo
1. Njoo kwangu Bwana Yesu Wangu katika ekaristi, kwa chakula cha mwiliyo nikashibishwe milele.
Iongoze nafsi yangu bwana katika njia zote, na kwa damu yako mimi nikaburudishwe milele
Najitoa kwako mwokozi (Yesu) nifikishe mbinguni,
Nipokee kwako eh bwana nifikishe mbinguni
Safisha moyo wangu Yesu nifikishe mbinguni,
Ongoza njia yangu Bwana nifikishe mbinguni
2. Najongea meza yako Bwana meza ya ukumbusho, ukumbusho wa chakula kitakacholiwa milele, itakase roho yangu bwana ili niistahili kula na kunywa katika karamu yako ee Yesu
3. Hata kama sistahili mimi bwana nakuhitaji,
Wewe ndiwe tabibu wa moyo wangu njoo kwangu bwana.
Nifikapo kwenye giza kubwa wewe ndiwe mwangaza, niangazie kipenyezi kinifikishe mbinguni
4. Usibaki nyuma ndugu yangu pia jitayarishe kumpokea mwokozi wako Yesu Kristu moyoni.Ewe kaka ewe dada yangu njoo huku hima hima, tushiriki kwa pamoja karamu ya bwana mwokozi
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu