Ingia / Jisajili

Nimeamini

Mtunzi: LUKRESIA MSELABUYE
> Mfahamu Zaidi LUKRESIA MSELABUYE
> Tazama Nyimbo nyingine za LUKRESIA MSELABUYE

Makundi Nyimbo: Tenzi za Kiswahili

Umepakiwa na: YOPASIA MSELABUYE

Umepakuliwa mara 1 | Umetazamwa mara 0

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

NIMEAMINI BY Lukresia Mselabuye

Verse 1.

Mungu ndiye muweza wa mambo yote eeeh

Nimechagua kuamini agabo lake kwangu

Japo kuwa napata vipingamizi

Nimechagua kusubiri ahadi zake kwangu

Wanayosema ni mengi kunirudisha nyuma

Lakini yote si kitu Nimesimama

Aliyotenda ni mengi Siwezi rudi nyuma

Siwezi kusimulia nikamaliza


Chorus!!

Soloist. Wote.

Kama Yesu ni mwanadamu. Sijui sijui sijui Ninasema

Ati Yesu mwana wa seremala. Sijui Sijui Sijui

Kama Yesu hakutoka kwa Mungu. Sijui sijui sijui Ninasema

Ati Yesu sio mwana wa Mungu. Sijui Sijui Sijui

Wote: Ninalijua moja nilikuwa kipofu sasa ninaona. ×2


Verse 2.

Ni Roho mtakatifu mwenye mapaji. iiiiiih

Nimechagua kutumaini nguvu zake kwangu

Ajuaye maana ya kila sauti

Nimechagua kuamini uwepo wake kwangu

Mwenye umungu mmoja na Mungu muumbaji

Mwenye ushirika kamili naye Yesu

Ninaamini ndani ya utatu mtakatifu

Ndipo napata uzima na nguvu tele


Chorus - Nalikuwa na dhambia nimesamehewa ×2


Verse 3

Eti kanisa usalipo sio la kweli iiiiih

Nimechagua kuamini kanisa moja tu

Kanisa katoriki na la mitume eeeeh

Msingi wake ndiye yesu mwokozi wetu

Alilojenga mwenyewe juu ya mwamba Petro

Nayo milango ya kuzimu haitashinda

Mashaka yao si kitu katika njia yangu

Nimeamini ninakiri Yesu ni Bwana


Chorus -Ninalijua moja nalifungwa na dhambi sasa nipo huru ×2



Verse 4

 Eti maisha ulonayo hayakufai iiiih

Nimechagua kuamini ahadi zake kwangu

Ati ugonjwa ulonao hautapona aaah

Nimechagua kuamini mapenzi yake kwangu

Kuishi kwangu ni kristo na kufa ni faida

Najua kufanikiwa pia kudhiliwa

Nimefundishwa kushiba pia kuona njaa

Imani yangu kwake Yesu nimeiweka.


Chorus. . Ninalijua moja nalikuwa kiwete sasa natembea ×2


KIBWAGIZO.

Kwa maana jinsi hii

Mungu aliupenda ulimwengu wote

Kamtoa mwanae wa pekee

Ili kila amwaminiye asipotee

Bali awe na uzima wa milele

Ni upendo gani huu nimepewa

Yesu afe kwa ajili yangu mimi

Nimekombolewa kwa damu ya thamani

Yesu si mwanadamu

Hafananishwi na kitu

Kajivua utukufu

Afe kwa ajili yangu

Yesu kwangu ni Mungu

Mwana halisi wa Mungu

Sitaacha kulisifu

Jina lake lake takatifu Daima

Sifa apewe Bwana, sifa apewe Yesu Kristo 

Sifa apewe Bwana Daima


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa