Mtunzi: LUCHAGULA NGASSA
> Mfahamu Zaidi LUCHAGULA NGASSA
> Tazama Nyimbo nyingine za LUCHAGULA NGASSA
Makundi Nyimbo: Kwaresma | Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: NGASSA LUCHAGULA
Umepakuliwa mara 2 | Umetazamwa mara 0
Download Nota Download MidiNimekukosea Ee Mungu wangu, nikitafakari maisha yangu, ninakuomba unihururumie×2
1. Dhambi zangu zilikutesa pale msalabani, hukuwa na kosa lolote pia majeraha uliyoyapata unihurumie ni upotovu wangu.
2. Nimelemewa na mizigo, ya dhambi zangu, zinanisononesha, nimekuwa mfungwa wa dhambi nioshe kwa damu yako.
3. Ninapotaka kutenda mazuri natenda mabaya, bila maongozi yako Bwana nitashindwa, nitapotea Mungu wangu niokoe.
4. Unisaidie niweze kuyavumilia mapungufu ya wenzangu, huku nikitambua ya kwamba hata mimi ninayo mapungufu, na unipe moyo wa kuomba radhi na kuwasamehe walionikosea.