Ingia / Jisajili

Ninakupenda Ewe Mwokozi Wangu

Mtunzi: Paschal Florian Mwarabu
> Tazama Nyimbo nyingine za Paschal Florian Mwarabu

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Eusebius Joseph Mikongoti

Umepakuliwa mara 11,078 | Umetazamwa mara 20,817

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kiitikio;

Ninakupenda Ewe Mwokozi wangu, rafiki yangu mpenzi wa moyo wangu

Ukae nami daima ndani yangu, nipate nguvu rohoni siku zote.

Mashairi;

1a). Ninakutolea mwili na roho yangu, uzipe neema zako nipate nguvu,

   b). Nikae nikupendeze Mwokozi wangu, shetani muovu kamwe asinifwate.

 2a). Nilinde niwe imara na mwenye nguvu, nisitumbukie tena katika dhambi,

  b). Unionyeshe yaliyo ya heri kweli, nipate kuishi kwa kumpendeza Bwana.
 
3 a). Wewe uliye njia kweli na uzima, niongoze vema daima siku zote,
   b). Uniangazie mwanga palipo giza, nifike kwa Mungu Baba kwa njia yako.
 
4 a). Nakukaribisha Bwana moyoni mwangu, nijalie baraka zako Ewe Bwana,

    b). Hata siku ya mwisho itapowadia, niite mbinguni kwenye heri milele.


Maoni - Toa Maoni

David Onyango Jul 06, 2022
Naomba mp3 wa huu wimbo

David Onyango Jul 06, 2022
Naomba mp wa huu wimbo

Geofrey Kanyambo Sep 08, 2021
Nomba MP3 ya wimbo huu ni mzuri sana

Daniel Dec 01, 2019
Nice song. Can I get mp3

Baltasar Remmy Temu Feb 19, 2019
Wimbo mzuri sana huu. Unatukumbusha zamani sana

Toa Maoni yako hapa