Mtunzi: Joseph H. Kabula
> Mfahamu Zaidi Joseph H. Kabula
> Tazama Nyimbo nyingine za Joseph H. Kabula
Makundi Nyimbo: Kwaresma | Mafundisho / Tafakari | Shukrani
Umepakiwa na: Thomas George Mwakimata
Umepakuliwa mara 1,119 | Umetazamwa mara 3,516
Download Nota Download MidiKatika Safari ya utimilifu wa maisha yangu Ee Bwana x 2. Uniongoze nishike mkono nisianguke, unifundishe unyenye kevu niwapende watu wote, Uniongoze Ee Bwana mimi ni mpofu nifike kwako salama, Ukae daima mwangu nipate nguvu nivuke shimo la dhambi.
Mashairi:
1. Kwa wingi wa huruma yako, kwa wingi wa fadhili zako, angaza giza la moyo wangu Ee Bwana na ufahamu wangu nitimize agano lako takatifu na la kweli.
2. Niepushe na yule mwovu, pamoja na hila zake asije kunipotosha mimi Bwana nisimame imara mwisho nifurahi pamoja nawe huko mbinguni.
3. Nipitapo kwenye hatari tegemeo langu ni wewe naomba Bwana usikae mbali nami unilinde Ee Bwana ili nipate kuwa salama daima milele.
Dunia ya sasa imejaa machafuko mengi Bwana kwa udhaifu wangu Ee Bwana nakusihi.
Uniongoze Ee Bwana Katika kweli yako, Unishike mkono Bwana katika kweli yako, Unijalie Ee Bwana imani thabiti, Ukae ndani yangu Bwana niwe salama, Ukae ndani yangu Bwana niishi kwa amani na mwisho nifike kwako Mbinguni