Ingia / Jisajili

Nitakapotakaswa Kati Yenu

Mtunzi: Beatus M. Idama
> Tazama Nyimbo nyingine za Beatus M. Idama

Makundi Nyimbo: Kwaresma

Umepakiwa na: Beatus Idama

Umepakuliwa mara 386 | Umetazamwa mara 1,606

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

NITAKAPOTAKASWA AKTI YENU

Nitakapotakaswa kati yenu, nitawakusanya na kuwatoa toka nchi zote

//: Nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtatakasika na uchafu wenu wote nami nitawapa ninyi moyo mpya asema Bwana://

1. Nitauondoa kwenu moyo mgumu kama moyo wa jiwe, nami nitawapa ninyi moyo wa utii; nitatia ndani yenu roho yangu; mtashika amri zangu na kuyazingatia maazimio yangu.

2. nchi iliyokuwa jangwa sasa imekuwa kama bustani ya Edeni, ile miji ya ukiwa, mahame na magofu sasa ni miji ya watu tena ina ngome ndipo nchi kando yenu watatambua mimi ni Mungu niliyejenga upya.

3. Mtakaa katika nchi niliyowapa baba zenu nanyi mtakuwa watu wangu. Nitaongeza mavuno wala sitaileta njaa. Nitazidisha matunda na mazao ya mashamba ili msiaibike, ili msiaibike kwa njaa kati ya mataifa.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa