Ingia / Jisajili

Nitakushukuru Bwana Mungu

Mtunzi: Inicent Nyombi

Makundi Nyimbo: Zaburi

Umepakiwa na: AUGUSTINE RUTAKOLZIBWA

Umepakuliwa mara 971 | Umetazamwa mara 3,686

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

  1. a) Mataifa wamezama katika shimo walilolifanya kwa wavu waliouficha imenaswa miguu yao.
    b) Bwana amejidhihirisha katika kuitekeleza hukumu, amemnasa mdhalimu kwa kazi ya mikono yake.

    Nitakushukuru Bwana Mungu kwa moyo wangu wote, nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu.
    Nitafurahi toka moyoni na kushangilia, nitaliimbia jina lako wewe uliye juu.
     
  2. a) Bwana Mungu tuokoe maana mcha Mungu amekoma,Maana uaminifu umetoweka kwa wanadamu.
    b) Husema yasiyofaa na tena kila mtu na mwenziwe Mengi ya kujipendekeza kwa mihoyo ya unafiki.
     
  3. a) Mpumbavu amesema moyoni hakika hakuna Mungu kwa kuyaharibu matendo yao na kufanya chukizo.
    b) Toka mbingu Bwana Mungu aliwachungulia wanadamu aone kama yuko mtu wa akili kumcha yeye.
     
  4. a) Nalikuwa ni kijana na mimi hivi sasa ni mzee lakini sijaona kamwe aliye haki ameachwa.
    b) Mwenye haki ni mfadhili hakika tena yeye anakopesha wazao watokae kwake wao pia hubarikiwa.
     
  5. a) Bwana Mungu umefanya kwa wingi miujiza mingi kwetu Hakuna wa kufananishwa na wewe muuumaji wetu.
    b) Ningependa kuyatangaza na kuyahubiri matendo yako Hayahesabiki ni mengi Ee Baba tunakushukuru.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa