Mtunzi: Robert Muriuki
Makundi Nyimbo: Shukrani
Umepakiwa na: Robert Muriuki
Umepakuliwa mara 563 | Umetazamwa mara 2,105
Download Nota Download Midi2. Umenilisha na umeninywesha
Wema wa mbinguni nimeupata,
Nashukuru Bwana u ndani yangu
3.Ukarimu wako na huruma yako,
Msamaha pia na upole wako,
Umenitendea wema wa ajabu.
4. Ndani yangu kweli Mwokozi yumo,
Hakika kwa mwili na damu yake,
Ni rafiki yangu sitamwacha kamwe.
5. Wema na fadhili itanifuata,
Siku zangu zote za maisha yangu,
Nami n'takaa ndani mwako daima.
6. Nitalieleza jina lako Bwana,
Nilitangaze kwa mataifa yote,
Wakuinue na wakushukuru.