Mtunzi: Joseph Rimisho
> Mfahamu Zaidi Joseph Rimisho
> Tazama Nyimbo nyingine za Joseph Rimisho
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Shukrani
Umepakiwa na: JOSEPH RIMISHO
Umepakuliwa mara 1,370 | Umetazamwa mara 4,385
Download Nota Download MidiKiitikio
Nitamuimbia Bwana Mungu wangu ningali hai,
Nitautangaza utukufu wake kwa mataifa
(NItavipiga vinanda, nitazicheza na ngoma, nitavicheza vinubi, nitalicheza na zeze (nami)
Nitasimulia maajabu ya Mungu kwa viumbe vyote) x2
Mashairi
1.(a). Katika kundi kubwa nitatangaza sifa zake,
(b). Nitamsifu kwa matari na kwa filimbi tamu, nitawaongoza watu wamtukuze Bwana Mungu wetu.
2. (a). Enyi jamaa za dunia msifuni kwa shangwe,
(b). Muimbieni Mungu wetu aliye juu mbinguni, mtukuzeni katika utakatifu na ukuu wake.
3. (a). Moyo wangu ni chombo kilichojaa sifa yake,
(b). Ulimi wangu utakiri matendo yake Mungu, na nafsi yangu itayasifia matendo yake Mungu wetu.