Mtunzi: Fr. Malili
Makundi Nyimbo: Ndoa
Umepakiwa na: Vusile Silonda
Umepakuliwa mara 4,866 | Umetazamwa mara 7,504
Download Nota
Download Midi
Maneno ya wimbo
Kiitikio:
Ona mnavyopendeza, ona mnavyometameta x 2
Wapenzi wana harusi mwende mkaishi salama x 2
Mashairi:
-
Kwenye maisha ya ndoa, kuna raha pia tabu, mkiishi kwa upendo tabu na raha ni sawa.
-
Mpendane siku zote, katika maisha yenu, msiruhusu shetani kuvuruga ndoa yenu.
-
Watoto mtakaopewa, muwatunze hao vyema, kwani kufanya hivyo Mungu mtampendeza.
-
Mjenge familia bora, yenye kuheshimu sala, kwani kwa njia ya sala tunaongea na Mungu.