Mtunzi: Michael Chima
> Mfahamu Zaidi Michael Chima
Makundi Nyimbo: Kwaresma | Mafundisho / Tafakari | Mazishi
Umepakiwa na: Derick Wafula
Umepakuliwa mara 635 | Umetazamwa mara 1,542
Download NotaPiga picha ndani ya moyo wako je, ukifika Mbinguni Mungu akakupokea na kukuambia Karibu Mwanangu, { Karibu Mwanangu (Karibu Mwanangu) nimekupokea kwa sababu ya Matendo yako mema }x2
1.Karibu Mwanangu mimi ndimi Bwana Mungu niliyekuumba, Ndimi Bwana Muumba wako Nimependezwa na matendo yako......-
(S/A) *Ishi mwanangu na watakatifu, ndilo taji nililoliandaa kwa ajili yako*
(T/B)
*Ishi Mwanangu pamoja na Watakatifu wote Mbinguni, ndilo taji mimi nililoliandaa liandaa kwa ajili yako*
2. Uliwasaidia Yatima, Wajane na wasio jiweza wote wenye shida mbalimbali, nimependezwa na matendo yako.....
Ishi Mwanangu na watakatifu_
.....
3. Wageni kwako walikula walikunywa walilala pazuri, uliishi nao kwa Upendo nimependezwa na matendo yako....... Ishi Mwanangu.....
4. Hata Maadui wako Ulishiriki nao kwa mambo mengi japo haukupendezwa nao nimependezwa na matendo yako..... *Ishi mwanangu*......