Ingia / Jisajili

Shangwe Kwa Mtoto Yesu

Mtunzi: Deogratius Dotto
> Mfahamu Zaidi Deogratius Dotto
> Tazama Nyimbo nyingine za Deogratius Dotto

Makundi Nyimbo: Noeli

Umepakiwa na: Deogratius Dotto

Umepakuliwa mara 63 | Umetazamwa mara 68

Download Nota
Maneno ya wimbo

Leo shangwe kuu imetanda ulimwenguni, kwani mkombozi wetu Bwana Yesu kazaliwa, leo, utukufu kwake Mungu nayo amani tele, kwani...

Sasa enyi watu wote pigeni (pigeni kelele za...)vigeregere

I. Shangwe kwa mtoto Yesu na vigeregere, ndelemo na chereko pia na vifijo, haya twende sote kule...

II. Sha-ngwe, vigeregere, ndelemo, na vifijo, twende, kule...

III. Mtoto Yesu, geregere, na chereko, na vifijo haya twende sote kule...

IV. Mtoto Yesu-, geregere, na chereko-, na vifijo...

Pangoni tukamwone mtoto Yesu amelazwa manyasini kule bethlehemu (pigeni kelele)X2.

1. Horini mtoto amelala (kalala kasinzia) malaika wanamtunza (kweli) amelazwa manyasini kule bethlehemu.

2. Nasi twendeni bethlehemu (pangoni bethlehemu) tukamuone mkombozi (twende) amelazwa manyasini kule bethlehemu

Ahaa-, shangwe kubwa-, kwa mtoto Yesu (Kristo leo kazaliwa tumepewa mtoto mwanaume) hee- shangwe kubwa- kwa mtoto Yesu na- uwezo wake kweli wa kifalme, ha!,

[Twende sote kule Bethle-hemu tukamu-one mtotoX2,

(Kina baba) twendeni, (nanyi kina mama) twendeni, (Na watoto wote) twendeniii kule, twendeni.

(Tuchukue) twendeni, (Dhahabu uvumba) twendeni, (Tunu manemane) twendeni kule Twendeni]X2. TWENDENIIIII


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa