Ingia / Jisajili

Siku ile Niliyokuita Bwana

Mtunzi: Ernest Magunus
> Mfahamu Zaidi Ernest Magunus
> Tazama Nyimbo nyingine za Ernest Magunus

Makundi Nyimbo: Zaburi

Umepakiwa na: ERNEST MAGUNUS

Umepakuliwa mara 512 | Umetazamwa mara 1,493

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

KIITIKIO:

Siku ile niliyokuita uliniitikia, Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.×2

MAIMBILIZI: (Zab. 137: 1-3, 6-9.)

1. Nitakushukuru kwa moyo wangu wote, Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi. Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu.

2. Nitalishukuru jina lako, Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako, Kwa maana umekuza ahadi yako, Kuliko jina lakolote. SikuileniliyokuitauliniitikiaUkanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.

3. Ingawa Bwana yuko juu, amwona mnyenyekevu, Naye amjua mwenye kujivuna tokeambali. Nijapokwenda kati ya shida utanihuisha, Utanyosha mkono juu ya hasira ya adui zangu.

4. Na mkono wako wa kuume utaniokoa. Bwana atanitimoliza mambo yangu; Ee Bwana, fadhili zako ni za milele; Usiziache kazi za mikono yako.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa