Ingia / Jisajili

SIKU TULIO INGOJA

Mtunzi: Samuel Msafiri
> Mfahamu Zaidi Samuel Msafiri
> Tazama Nyimbo nyingine za Samuel Msafiri

Makundi Nyimbo: Ndoa

Umepakiwa na: Samuel Msafiri

Umepakuliwa mara 691 | Umetazamwa mara 1,839

Download Nota
Maneno ya wimbo
SIKU TULIO INGOJA K: Siku hii tulio ingoja sasa imetimia leo, ni shangwe kubwa siku hii ya leo kaka na dada wa ungana. tuimbe tucheze tufurahie na tushangilie. 1. Nitakupenda mme wangu kwa moyo wangu wote, mimi ni mwanadamu wala sijakamilika, nivumilie kwa mapungufu yangu yote utakayo yaona. T+B: Hio ni kweli mke wangu, wewe hukamiliki nitavumilia yote nitakayo ya ona. 2. Naku ahidi mme wangu nitakulinda mimi kwa raha pia tabu afya pia magonjwa, nitakupenda, kuku heshimu siku zote za maisha yangu. T+B: Pia mimi naku ahidi nitakulinda wewe kwa raha pia na tabu nitakuwa nawe. 3. Baba mama kaka dada na marafiki zangu ninyi nimashahidi wa ndoa hii, mtuombee kwake Mungu atulinde maishani mwetu T+B: Mtu ombee kwake Mungu kwa pendo letu hili, tuzae watoto wenye maadili mema. 4. Siku tizama sura wala uwezo wako, nilicho penda kwako nitabia yako na upole na ukarimu ndio kweli ulio nivutia. T+B: Naku ahidi mke wangu wala sibadiliki , wala huto jutia kunipenda mimi.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa