Ingia / Jisajili

Tajiri Na Maskini Razaro

Mtunzi: Kakoyo Damian Aureus Msuha
> Mfahamu Zaidi Kakoyo Damian Aureus Msuha
> Tazama Nyimbo nyingine za Kakoyo Damian Aureus Msuha

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Damian Msuha

Umepakuliwa mara 626 | Umetazamwa mara 1,871

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Utangulizi.

Palikuwa na tajiri aliyevaa nguo za zambarau, na kitani safi na kula kwa anasa siku zote. Na maskini Razaro mlangoni pake aliyekuwa na vidonda vingi, na kula kwake ni makombo ya tajiri hata mbwa akalamba vidonda vyake.

Kiitikio.

Basi ikawa tajiri alikufa na Razaro alikufa ndipo kuzimu tajiri akafumbua macho, akiwa katika mateso makali alimwona Ibrahimu kwa mbali na Razaro kifuani mwake. Akalia akasema Ee baba Ibrahimu unihurumie ninaangamia kwa sababu ninateswa katika moto huu, Ibrahimu aksema mwanangu kumbuka uliyapokea mema yako duniani na Razaro mabaya sasa yuko hapa na zaidi ya hayo, (kumewekwa shimo kubwa kati yetu sisi nanyi  shimo kubwa linalotutenganisha x2)

Mashairi

  1. Akasema basi baba umtume Razaro nyumbani kwa baba yangu awashuhudie wasije wakafika mahali hapa pa mateso
  2. Ibrahimu akasema wanao musa na manabii wawasikilize wao.
  3. Akasema bali baba wakiwaendea mtu atokaye kwa wafu hakika watatubu
  4. Ibrahimu akamwambia wasipowasikia musa na manabii, hawatashawishiwa hata mtu akifufuka katika wafu.

Maoni - Toa Maoni

Sifael Oct 02, 2024
Nashukuru sana kwa maelezo haya nimejifunza jambo.... Barikiwa sana

Toa Maoni yako hapa