Ingia / Jisajili

Tazama Ninawatuma

Mtunzi: Beatus M. Idama
> Tazama Nyimbo nyingine za Beatus M. Idama

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Beatus Idama

Umepakuliwa mara 356 | Umetazamwa mara 2,181

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

TAZAMA NINAWATUMA

Tazama ninawatuma kama kondoo kati ya mbwa mwitu - hivyo muwe werevu kama nyoka na wapole kama hua.

Tazama ninawatuma kama kondoo kati ya mbwa mwitu - hivyo muwe werevu kama nyoka na wapole kama hua.

Jihadharini nao wanadamu kwa maana watawapeleka mabarazani mwao na kuwapiga kwenye masunagogi, masunagogi yao.

Nanyi mtaburutwa mbele ya watawala na wafalme - mtaburutwa kwa ajili yangu iwe ushuhuda kwao na mbele ya watu wa mataifa;

Lakini watakapowapeleka humo msisumbuke kufikirifikiri kwamba ni nini mtapaswa kusema kwa maana mtapewa la kusema;

//:Kwa sababu si ninyi mtakaokuwa mkinena - bali ni Roho wa Baba yenu ndiye atakayenena kupitia kwenu://


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa