Maneno ya wimbo
TAZAMA UWINGUNI
Tazama uwinguni tazama anakuja mfalme wa wafalme ndiye kristu mwokozi,
Ajaye ni mtawala mwenye nguvu na enzi, kristu mfalme mwenye utukufu na enzi.
1.Kristu mchungaji mwema ana fimbo mkono kuwalisha kondoo wa malisho yake,
(tujitayarisheni tuingie katika kundi moja la kondoo wa malisho yako)*2
2.Kristu mwenye mamlaka ana funguo zake kuwafungua wote wale waliofungwa.
(Tujitayarisheni tutubu dhambi zetu roho zetu ziwe safi ajapo aingie)*2
3.Kristu jaji mkuu ana hukumu zake, kuwahukumu wazima pia nao wafu,
(Tujifunze upendo pia unyeyekevu tuishi kwa amani tukisaidiana)*2
4.Tumwimbie mfalme tumfanyieni shangwe tumshukuruni kwa nyimbo nzuri za furaha
(Tumwimbieni mfalme tumfanyieni shangwe tumshukuruni kwa nyimbo nzuri za furaha.
(Tupigeni makofi pia vigelegele tumsifu leo kesho na milele amina)*2