Mtunzi: Rwebangira, P. G.
> Tazama Nyimbo nyingine za Rwebangira, P. G.
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio
Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela
Umepakuliwa mara 559 | Umetazamwa mara 2,612
Download Nota Download MidiWaamini tujongeeni mezani pake tukampokee mwokozi Yesu x2
Yeye ametualika kwa karamu ya mwili wake pia damu yake x2
1. Kwanza tujitakase mioyoni mwetu ndipo tuijongee karamu yake
Karamu ya upendo tena ya amani wana heri waliopata mwaliko
2. Twendeni tushiriki chakula cha mbingu shibe ya roho zetu wana wa Mungu
Pia tunywe kinywaji damu ya mwokozi roho zetu zipate kuburudika
3. Maana waliyokula mababu jangwani ilikuwa mkate siyo uzima
Chakula tukilacho ndicho cha uzima karibu jongeeni mpate uzima