Mtunzi: Charles Saasita
> Mfahamu Zaidi Charles Saasita
> Tazama Nyimbo nyingine za Charles Saasita
Makundi Nyimbo: Majilio
Umepakiwa na: FORTUNE SHIMANYI
Umepakuliwa mara 7,406 | Umetazamwa mara 11,149
Download Nota Download Midi1.Tunamtazamia mwokozi; Bwana Yesu Kristo atakaye ubadili mwili wetu wa unyonge upate kufanana na mwili wake wa utukufu. Tunamtazamia mwokozi.
2.Tunamtazamia mwokozi; Bwana Yesu Kristo atakaye tuchukua kwenda nyumbani kwa Baba, tukae naye milele yote tukimsifu kwa nyimbo. Tunamtazamia mwokozi.
3.Tunamtazamia mwokozi; Bwana Yesu Kristo atakaye tulipia yote tulodhulumiwa, tusije pungukiwa lolote kwa kumfuata yeye. Tunamtazamia mwokozi.
4.Tunamtazamia mwokozi; Bwana Yesu Kristo atakaye kuja kwetu kwa utukufu na enzi, apate kuhukumu wazima na walio mauti. Tunamtazamia mwokozi.
5.Tunamtazamia mwokozi; Bwana Yesu Kristo yeye Alfa na Omega, ni wa kwanza na wa mwisho aja kulitimiza agano lilowekwa milele. Tunamtazamia mwokozi.