Ingia / Jisajili

Tunzeni Kiapo Chenu

Mtunzi: Peter Mboye
> Tazama Nyimbo nyingine za Peter Mboye

Makundi Nyimbo: Ndoa

Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela

Umepakuliwa mara 13,620 | Umetazamwa mara 17,789

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kiitikio:

(Wanandoa) tunzeni kiapo chenu x 2
Mlisema mwapendana, mtaheshimiana, mtavumiliana, mtasaidiana x 2

Mashairi:

  1. Mliahidi mbele za Mungu kuishi pamoja, katika shida, katika raha, msikubali yule muovu awatenganishe, mshikamane, mfike mwisho.
  2. Hebu tazama huyo mwenzako alivyo mzuri, umthamini, utampenda, ukitembea barabarani usitoe macho, hakuna tena, zaidi yake.
  3. Wafundisheni watoto wenu wamjue Mungu, Mungu mmoja, muumba vyote, mkifaulu zawadi yenu ni kubwa mbinguni, mtafurahi, milele yote.

Maoni - Toa Maoni

Justine Nov 07, 2017
hii nyimbo ni kiwango cha lami,my wife anaipenda mpk anaoza asee.....tih.

Casimir Mahimbo Nov 06, 2017
Wimbo huu kiboko, daima napenda kuusikiliza na kucheza

Joseph M Ndimila Oct 05, 2017
Wimbo huu ni mzuri sana kati ya nyimbo zote za ndoa huu ndo naupenda zaidi. Hongera sana mtunzi na Mungu akubari

Justina Peter Jun 16, 2017
Wimbo mzur sn, mzur mno una msg nzr melody yake nzr mno...Hongera sn mtunz...nyimbo zako zote ni nzr mno, kwel znanibarik

andrew john Feb 14, 2017
nimeupenda sana huu wimbo hongera sana mtunzi

May 10, 2016
Wimbo huu kwa kweli nimeupenda hasa melod yake ipo vizuri.Hongera sana mtunzi

Toa Maoni yako hapa