Mtunzi: Siahi Denis
Makundi Nyimbo: Pentekoste | Miito | Ubatizo | Utatu Mtakatifu | Watakatifu
Umepakiwa na: Giulio Mukaathe
Umepakuliwa mara 614 | Umetazamwa mara 2,313
Download Nota
Maneno ya wimbo
WIMBO:Uje roho mtakatifu.
MTUNZI:Siahi Denis
CHOIR:Kwaya ya Maria Kikao cha Hekima Chuo kikuu Masinde Muliro Kenya
Kiitikio:
Uje ewe roho mtakatifu uzijaze roho zetu, uje kwetu ewe mfariji ututie faraja zako.
Ututie pendo lako, tuwapende ndugu zetu, na amani tujalie tuishi kwa amani yako.
Zienee nyoyo zao waumini wote kweli,uwatie mapendo yako ewe roho mwema. ( x2)
1.Roho uliye mfariji wa wajane,tena uliye mfariji wa yatima, tunakuomba uwashushie faraja zako,Uwafute machozi ewe roho mungu njoo.
2.Tufungulie siri za mbingu zilizofichwa,tujue ukweli wa rehema zake, tukupende mungu wetu,tukutumikie,tuwapende ndugu zetu kama nafsi zetu.
3.Wewe uliyewashukia wanafunzi wako,ukawaunganisha kwa lugha mbalimabali,wakasema matendo makuu ya mungu,uje kwetu roho mwema, ewe roho mungu njoo.
4.Wape waamini wako mapaji yako,tujalie sisi mwanga wenye heri,utujaze neema zako mioyoni,tuyatende ya kupendeza bwana mungu wetu.