Ingia / Jisajili

Uovu Umenitenda

Mtunzi: Innocent Fundisha

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela

Umepakuliwa mara 575 | Umetazamwa mara 1,569

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
  1. Sikitiko kubwa linajiinua nikiikumbuka hukumu yako.
    Nilifurahia mambo ya dunia kwa kiburi nikakudhihaki.

    Natetemeka kwa hofu kuu na kuzimia giza limeshika hatamu uovu wangu umenitenda x 2
     
  2. Nimekukosea kwa ukaidi wangu, nakujifanya mwamba mbele zako.
    Sistahili tena kuwa mwanao, msamaha wako uniangukie.
     
  3. Mwisho wa maisha yangu nauona, nitasema nini nitakwenda wapi.
    Uamuzi wangu ni kukaa kimya, Nikiisubiri huruma yako.
     
  4. Shukrani zangu zikufikie, Bwana Yesu Kristu mfalme wa Amani.
    Uliniumba kwa mfano wako, ukanipa vyote nivitawale.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa